Kitabu
hiki cha maisha halisi ya mtoto wa mtaani ni ushuhuda wa kweli wa JAMES
YUSTAR JUSTINE EBRANIA, aliyeokotwa jalalani na baada ya safari ndefu
ya maisha yake toka kuokotwa kwake, kupitia mazingira magumu hatari na
yenye misukosuko mingi. James aanza maisha mapya na kuweka historia kati
ya walioshinda maisha ya kuitwa watoto wa mitaani.
Kitabu
hiki kinatoa Taswira ya mabadiliko kwa jamii iliyokata tamaa pia
kinaelezea mazingira halisi ya watoto wa mtaani, matatizo na maisha
magumu wanayoyapitia kama unyanywasaji, njaa, vifo, majeraha, hata
ulemavu wa kudumu, ukosefu wa elimu, huduma muhimu, ukosefu wa elimu,
hudumu muhimu za kijamii kama matibabu na malazi bora.
Kwa
kupitia kitabu hiki kinachoelezea maisha halisi ya James Yuster
kinaonyesha kwa hisia jinsi watoto wa mtaani wanavyojihisi / kujiona
kuwa jamii imewatenga wananyanyapaliwa na kujihisi upweke, kana kwamba
hawana haki ya kuhishi pamoja na jamii hapa Duniani.
Pia
utapata kuona jinsi hawa watoto walivyosahaulika katika jamii na
kupoteza thamani ya utu wao, jamii inawachukulia kama wezi, wahuni,
watumiaji wa dawa za kulevya, ulawiti na kuonekana kama viumbe wa ajabu
machoni mwao.
Kupitia
kitabu hiki jamaii itajifunza madhara ya utoaji mimba na utupaji wa
watoto ambao hupelekea ongezeko la watoto wa mtaani, hivyo nivyema jamii
ikaelimika na kushiriki katika kupunguza kundi kubwa la watoto
wanaoishi katika mazingira magumu.
-------------------------------------------------------------
This book on the real-life story of a street child is a true testimony of JAMES YUSTAR JUSTINE EBRANIA,
who was found abandoned at a dumpsite. After a long and difficult life
journey—facing dangerous and challenging circumstances—James eventually
began a new life and made history as one of the few who overcame the
label of a street child.
This book offers a vivid
portrayal of transformation for a society that has lost hope. It also
describes the harsh reality faced by street children, including abuse,
hunger, death, injuries, even permanent disabilities, lack of education,
and the absence of essential social services such as healthcare and
proper shelter.
Through this book, which
narrates the true experiences of James Yustar, readers will emotionally
connect with how street children feel neglected, stigmatized, and
isolated—as though they have no right to exist within society.
You will also see how these
children are forgotten by society and stripped of their dignity. They
are often perceived as thieves, troublemakers, drug addicts, or victims
of sexual abuse, and viewed as strange beings in the eyes of many.
This book also aims to
educate society on the consequences of abortion and child
abandonment—factors that contribute to the increasing number of street
children. Therefore, it is vital for communities to be educated and
actively involved in reducing the population of children living in
vulnerable conditions.
0 Comments